Analojia Tatu za Maisha ya Kikristo: Nyaraka za Mtume Petro #33

1st Petro 2:1-10

Na Dr. Robert Dean Luginbill
Wa https://ichthys.com

Tafsiri ya Kiswahili na Respicius Luciani Kilambo

Ruksa ya Tafsiri Hii Imetolewa Mahususi na Dr. R. D. Luginbill
Permission for this Kiswahili Translation has Been Kindly Granted by
Dr. R. D. Luginbill

Utangulizi: Baada ya kutafiti na kuelezea hadhi yetu kama waumini waliozaliwa upya kwa imani katika Injili, yaani Neno la Mungu, katika sura ya kwanza, na baada ya kuuelezea kwa uthabiti kabisa katika sura hiyo hiyo ya kwanza msingi kwamba hadhi hii iliyobarikiwa inatuamuru/inatulazimu tufanye maendeleo ya kiroho kwa namna ile ile [kama] tulivyoamini, na kwamba tuongeze katika/juu ya utakaso ule wa mwanzo, mwenendo mtakatifu wa maisha, Petro anaenda sasa katika hii sehemu ya kwanza ya sura ya pili kutufundisha kuhusu michakato ya kukua kiroho, maendeleo ya kiroho, na utumishi wa kiroho, kwa kutumia analojia (analogy - mifanano) tatu. Baada ya kwanza kutukumbusha juu ya ulazima wa mwenendo uliotakaswa ili tuweze kufanya maendeleo yoyote katika maisha yetu ya Kikristo (1Pet. 2:1), Petro anauelezea mchakato wa kukua kiroho kwa kutumia analojia ya mtoto anayekua (1Pet. 2:2-3), mchakato wa maendeleo ya kiroho kwa kutumia analojia ya ujenzi wa nyumba (1Pet. 2:4-8), na mchakato wa utumishi wa kiroho kwa kuulinganisha na ule utumishi wa makuhani wa Kilawi/Walawi (1Pet. 2:9-10). Tukitazama kwa uangalifu dondoo za kile anachokisema Petro hapa tutapata umaizi/ujuzi wa thamani kuu kuhusu mambo muhimu ya jinsi kila Mkristo anavyopaswa kuishi baada ya wokovu.

2.1 Basi (kwa kuwa Neno la Mungu ndilo msingi wa mema yote), [baada ya kuweka] mbali uovu [ubaya] wote na hila zote, na unafiki [wote] na husuda [zote] na masingizio [kashfa] zote.
2.2  Kama watoto wachanga waliozaliwa, sasa yatamanini maziwa ya [Neno yasiyo na udanganyifu], ili kwa hayo mpate [kukua katika] wokovu;
2.3  ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili [kwani] mmeonja ukweli kwamba Bwana [wetu] ni bora sana].
2.4 [Mmemwendea Yeye], jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali [katika macho ya] Mungu [Baba] ni teule, lenye heshima [kuu].
2.5 Ninyi wenyewe [pia], kama mawe yaliyo hai, mnajengwa [na Roho Mtakatifu] ili muwe nyumba ya kiroho, muwe makuhani watakatifu kwa ajili ya kutoa dhabihu za kiroho zinazomfurahisha Mungu kwa njia ya [Bwana] Yesu Kristo.
2.6 Hii ndiyo maana imeandikwa, “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe kuu la pembeni [la msingi], teule, lenye thamani/gharama kuu, naye amwaminiye Yeye kwa hakika hataingia katika aibu” - (nukuu kutoka Isa. 28:16).
2.7 Heshima hii ni yenu ninyi mnaoamini, lakini kwa wale wasioamini, [maandiko yanasema], “jiwe walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu la Msingi”,
2.8 na [limekuwa] “Jiwe la kujikwaa, Mwamba wa kuangusha”, nao hugongana dhidi ya Jiwe hili , kama walivyopangiwa [na Mungu] (kwa sababu ya uamuzi wao wa kumkataa Kristo).
2.9 Bali ninyi ni jamii teule, makuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki [wanaolindwa na] ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake adhimu;
2.10 ninyi ambao hapo mwanzo hamkuwa taifa,
lakini sasa mmekuwa taifa la Mungu;
ninyi ambao hapo mwanzo hamkupata rehema,
lakini sasa mmepata rehema.
1Petro 2:1-10

Utakaso Katika Maisha, Baada ya Wokovu: Sura ya pili ya waraka wa Petro inaanza na kibwagizo/kiitikio cha msingi wa utakaso katika maisha baada ya wokovu ambao Petro aliuzungumzia kwa undani kabisa (na ambao tumejifunza) katika sura ya kwanza. Muhtasari umeandikwa kwa utondoti (yaani kinaganaga), lakini kama ilivyo katika orodha nyingine za mwenendo mbaya ambao unapaswa kuepukwa na Wakristo (kw. mf. Waga. 5:19-21), haujakusudiwa kuchukuliwa kama orodha iliyokamilika (maana yake kuna makosa mengine ambayo hayajatajwa katika orodha hii, kwani Mkristo halisi au aliyepevuka ataongozwa katika kutambua mwenendo sahihi, na hafuati orodha ya fanya-hili, usifanye-lile [pekee]). Kwa maneno mengine, Petro hatosheki tu na kutukumbusha kwamba kutokana na nafasi yetu katika Kristo sisi ni “watu watakatifu”, na kwamba hilo linamaanisha kwamba tunapaswa kujitahidi tunavyoweza kuishi katika namna ya utakatifu zaidi na zaidi, siku hadi siku, Petro anaona haja ya – akiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu – kuweka orodha hapa, tusije tukajiona kwamba tumekwishafanikisha mwenendo mtimilifu wa Kikristo. Petro anafanya hivi si kwa makusudi ya kutukatisha tamaa (tunafahamu fika kwamba tunasamehewa makosa yetu yote mara tunapokiri makosa yetu kwa Bwana {1Yoh. 1:9}, na tunaweza kuwa na uhakika kwamba kama tunafanya kazi nzuri ya kujiweka mbali na dhambi – hasa dhambi nzito – basi hakuna haja ya kuumiza mioyo yetu kupita kiasi), bali kutukumbusha juu ya hulka danganyifu ya dhambi pamoja na wigo wake mpana, na unavyopenya katika maisha ya wanadamu (yaani hatubadiliki na kuwa watimilifu baada ya wokovu: 1Wafa. 8:46; Ayubu 15:14; Zab. 143:2; War. 3:23; 5:12; 5:12; 1Yoh. 1:8-10); Petro anafanya hivi, kwa maneno mengine, ili kutusaidia tuendelee kuwa wanyenyekevu katika suala hili, hata kama “tutafanya vyema tu” katika juhudi zetu binafsi za kuishi maisha matakatifu, yaliyotakaswa, yanayompatia heshima Bwana wetu Yesu Kristo.

Baada ya Kuweka Pembeni: Pia ni muhimu kuona/kutambua kwamba kurudia kuutizama tena msingi huu wa utakaso kwa kuliweka suala hili katika mtazamo wa matumizi yake, yaani kwa kutupatia mifano ya mambo gani ya kutofanya katika maisha yetu, kunatangulia mafundisho ya Petro ya yale yaliyo muhimu kwa ajili ya kukua kiroho kwa nia na matendo thabiti, na hivyo kuudhihirisha msingi ambao mara kadhaa tumeusisitiza, kwamba “kulinda goli na kushambulia goli la timu pinzani”, au kwa lugha ya kivita “kuimarisha ulinzi wa eneo lako na kushambulia eneo la adui” [vinaenda pamoja] na ndio mkakati ulio sahihi, kwani mapungufu katika upande wowote kati ya hizo sehemu mbili utaathiri vibaya ule upande wa pili. Ili kupata faida kubwa zaidi kutokana na maisha ya Kikristo na kumpa heshima au kumu-enzi Bwana wetu kwa uwezo wetu wote, ni lazima, siyo tu kuwa na mwenendo mtakatifu pekee au kukua, kuendelea na kuzaa matunda mema pekee – tunahitaji kufanikisha vyote, kwa sababu kufanikisha kimoja wapo bila [kufanikisha] kingine hakutatupeleka mbali na kutaathiri mchakato mzima [hatimaye]. Hili linaainishwa na matumizi ya Petro ya neno apothemenoi la Kiyunani katika wakati (tense) unaoendelea (participle), neno ambalo tunalitafsiri kama “tunavyoweka pembeni/kando”. Tunapaswa kutambua kuwa hili linahitaji maamuzi na matendo ya makusudi kabisa kwa upande wa muumini. Halitokei *“kwa ajali-ajali tu” wala “halijipi lenyewe” (it is neither accidental nor automatic). Zaidi ya hapo, kuachana na matendo mabaya ambayo Petro anaorodhesha hapa (pamoja na mwenendo wowote mwingine wa uovu) kunalazimu kiasi cha kutosha cha kupevuka kiroho. Ili kuwa na ufanisi katika kujizuia na dhambi ya aina yoyote, tunahitaji kujua kwa kiasi cha kutosha dhambi ni nini, kwani kama orodha hii inavyoonyesha, kuna sehemu kubwa katika eneo la fikra zetu na kauli zetu, kwa mfano, ambayo ina mwanya mkubwa wa dhambi pia. Kutekeleza amri ya Petro anayoitoa [akiwa] katika Roho Mtakatifu, tunahitaji pia kufahamu kwa kiasi fulani jinsi tulivyoumbwa, roho na mwili, hulka ya dhambi tuliyo nayo, vita ya kiroho tunayopigana wakati wote, jinsi ya kurudi katika hali ya utakaso baada ya tendo la dhambi, na kwa hakika kuhusu kila taswira ya ile kweli ya Neno la Mungu kwa sababu mafanikio katika kuishinda dhambi yanawezekana tu katika mtazamo timilifu wa kimungu katika kila kitu. Kwani wakati tunapojitoa (kwa sababu yoyote ile) kutoka kwenye mtazamo huo timilifu “wa kimungu” ndipo uwezekano wa kuangukia katika njia za kidunia za kufikiri, kuzungumza na kutenda unakuwepo.

2.15  Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba [kwa uhalisia] hakumo ndani yake.
2.16  Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima [yaani majigambo ya alicho nacho na anayoyafanya], havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

*Accident: jambo la “kubahatisha” - kwa hakika, hakuna “ajali”, hakuna “bahati” katika uumbaji/ulimwengu. Ajali, bahati, nasibu ni mafundisho ya Shetani.
2.17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu [akiwa hai] hata milele.
1Yoh. 2:15-17

Uovu wa Kila Aina: Uovu si tafsiri nzuri ya neno la Kiyunani kakia katika aya ya kwanza kwa sababu ni neno lenye "harufu" katika Kiswahili. Mahala popote utakapoliona neno "uovu" katika Agano la Kale, kwa mfano, karibu wakati wote ni tafsiri ya neno la Kiebrania "ubaya" (kama kinyume cha wema/uzuri), na ijapokuwa kuna neno lingine la Kiyunani linalomaanisha "uovu" (poneria), nalo pia linamaanisha "ubaya" katika kiini chake bila ya kuwa na viashiria/vidokezo vya neno letu la Kiswahili "uovu", na hivyo kakia ndilo neno ambalo linafaa hapa, ambalo tutalitafsiri kama "ubaya". Ikumbukwe kwamba kakia na poneria ni visawe (synonyms). *Tafsiri kadhaa za Kiingreza zinatumia neno "malice" kama tafsiri ya kakia, (ubaya), na hii si tafsiri mbaya, lakini neno hili – malice – halieleweki vizuri sana, na lina "harufu" ya mtazamo wa kifikra ulio "hasi" zaidi, wakati neno la Kiyunani tulilo nalo hapa linahusisha kiujumla jambo lolote lililofikiriwa, lililosemwa, na lililofanywa ambalo ni "baya" au ambalo ni dhambi. Tafsiri ya Kiingereza ya ASV – American Standard Version – inatumia neno "wickedness" ambalo pia linapoteza maana kwa sababu hata watenda dhambi wakubwa wanaweza kujiona wao si "wicked" – kwani ni neno ambalo lina maana za ziada za uovu wa kishetani, nguvu za giza, n.k. - na kakia ni neno ambalo halina maana mahususi kama hizo. "Sinfulness" ni neno linalokaribia katika maana kwa "badness – ubaya", lakini neno analolitumia Petro, kakia, halihusiani na neno la Kiyunani linalohusiana kimofimu (morpheme) na neno dhambi (ambalo ni hamart), ambalo angeweza kulitumia kwa urahisi tu. Bila shaka alijizuia kutumia neno hamart ambalo mofimu yake inahusiana na dhambi kwa sababu vinginevyo agizo hili lingekuwa haliwezekani kutekelezeka, kwani "sote hujikwaa mara moja-moja kiasi kwamba hata Mkristo aliyeendelea sana hawezi kuwa bila dhambi (Muhu. 7:20; War. 3:9; 3:23; 7:14; 7:23; Waga. 3:22; Yak. 3:2; 1Yoh. 1:6-10; cf. Zab. 143:2). Hivyo neno "ubaya" linafikisha ujumbe hapa: wazo lolote, neno lolote, tendo lolote lisilofaa kwa Mkristo.

Kwa kutumia msemo "ubaya wote", Petro pia anayaweka mambo katika hali ya ujumla-jumla ili tuweze kuelewa kwamba utakaso unapaswa kujumuisha kila taswira au kila upande wa maisha ya muumini. Kwa kweli haiwezekani kuorodhesha kila aina ya dhambi inayoweza kutendwa, na kwa sababu hii hakuna hata orodha moja kati ya zote zilizomo katika maandiko zilizokusudiwa kuchukuliwa kuwa zimekamilika bali zinapaswa kueleweka kama vielelezo vya aina za mwenendo tunaoamriwa kujiepusha nao (kwa mfano 1Wakor. 6:9-10; Waga. 5:10-21; Waefe. 5:3-5)1. Kila kitu tunachokiwaza, tunachokisema na tunachokitenda. Kwani tunachokitenda kinasababishwa na tunachokisema na hicho kwa upande wake huongozwa na kile tunachokiwaza.

*Mfano KJV, NIV, ESV, n.k.
15.17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
15.18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
15.19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
15.20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
Matt. 15:17-20 SUV

Hivyo, fikra adilifu moyoni ndio ufunguo wa mwenendo uliotakaswa, ambao unalindwa na lugha/kauli njema iliyotakaswa, ambayo nayo inalindwa na mawazo matakatifu. Hii ndiyo maana ulimi unatiliwa mkazo katika mazungumzo ya namna hii kwa sababu ulimi unashika nafasi ya katikati kati ya nyanja hizi mbili, ukitangulia matendo na ukifichua mawazo:

3.2 Maana twajikwaa [mara nyingi twatenda dhambi bila kukusudia, kwa kughafilika] sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia [kuutawala] na mwili wake wote kama kwa lijamu [hatamu].
3.3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili watutii, hivi twageuza mwili wao wote [upande huu na huu].
3.4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
3.5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
3.6 Nao ulimi ni moto [kama huo]; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile [yaani, huwasha moto katika taswira za mfumo mzima wa wanadamu], nao huwashwa moto na jehanum.
3.7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
3.8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
3.9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
3.10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
Yakobo 3:2-10 SUV

Hila Zote: Neno la Kiyunani dolos maana yake ni ghiliba ya aibu, udanganyifu au ulaghai. Kama ilivyokuwa kwa "ubaya" (na kama itakavyokuwa katika mwisho wa orodha hii na "uzushi, kashfa"), Petro anaongeza kivumishi au ki-sifa "-ote" hapa kwa ajili ya kutia mkazo ili kusisitiza kutokukubalika kwa Mkristo yeyote anayeenenda katika namna ya udanganyifu. Mbinu za namna hii haziwezi kuhalalishwa katika mahusiano yetu na waumini wenzetu au hata wasioamini. Ijapokuwa yaweza kuwa kweli katika ulimwengu kwamba *vyote ni halali katika mapenzi na vita – na udanganyifu ni sehemu muhimu ya maarifa ya kivita – unafiki/undumakuwili, ulaghai na kujifanya/kujidai uko hivi kumbe sivyo, havina nafasi katika ule unaopaswa kuwa ni mwenendo wa heshima wa Mkristo kwa waumini wenzake na hata kwa wasioamini. Ukweli usioepukika ni kwamba mbinu za udanganyifu zinaficha motisha zisizostahili – ama zina uwezekano wa kumpeleka muumini katika hali ya kuwa na motisha za namna hiyo hata kama alikuwa "na nia njema". Mbinu hizi zinaweza kuwa halali tu ikiwa, kama tulivyogusia mwanzo, tuko katika vita na/au tunakabiliwa na uhalifu (yaani tunalazimika kutumia mbinu zozote tunapokabiliwa na jambazi, mtekaji nyara, muuaji au wakala yeyote wa adui). Lakini katika mazingira yetu ya kawaida, itakuwa vyema tukikumbuka maneno ya sifa ya Bwana wetu kwa Nathanaeli: "tazama, Mwizraeli kwelikweli, hamna hila ndani yake!" (Yoh. 1:47).

Unafiki [Wote]: Neno la Kiyunani hapa, ambalo kutokana nalo tunapata neno la Kiingereza "hypocrite", maana yake ya asili ni "mwigizaji". Hivyo unafiki ni kujifanya hivi kumbe siyo, kama ilivyokuwa kwa ule unafiki wa fedheha wa Mafarisayo ambao walijifanya wapendwa wa Mungu na watimizaji wa Sheria lakini kiuhalisia walikuwa wakijipenda [wao wenyewe] binafsi na wakiitumia Sheria kwa faida yao wenyewe. Petro anatumia neno unafiki katika uwingi (plural) – hypocrisies – ili kutia mkazo kwa kiasi fulani, lakini pia ili kutuelewesha sisi kwamba hii si nadharia tu bali pia ni mkusanyiko wa tabia mbaya – dhambi ambazo tunapaswa kujiepusha nazo. Wakati wowote ule tunapojipa sifa ambazo siyo zetu, au tunapojisifia jambo ambalo hatujalifanya, au tunapojihusisha na mwenendo wowote ambao ni wa kujionyesha tu, tunajiweka katika hatari ya kuwa wanafiki, kwa viwango vinavyofundishwa, [vilivyowekwa] na Biblia. Hivyo huu mwenendo hasi wa unafiki tunaopaswa kujiepusha nao unajumuisha zaidi ya kuwatazama wenzetu kwa kiwango tofauti na tunavyojitazama sisi wenyewe; unajumuisha pia "kufanya maigizo" ya aina yoyote mbele za wengine ili tuonekane katika mwanga tofauti na vile tulivyo kiuhalisia ndani yetu, ni jambo la kuepuka. Wakristo wanaotembea katika upendo halisi hawatakuwa na tatizo katika kuonyesha taswira ya wema halisi kwa sababu ndani ya roho zao wako "wema" kiuhalisia, wakitiwa nguvu na Roho Mtakatifu. Kusimika sura ya kinafiki, kwa upande mwingine, hakumsaidii mtu yeyote, pamoja na sisi wenyewe, na kwa kweli kunaweza kutuletea madhara makubwa kwa sababu katika kiini chake ni mwenendo wa uwongo/udanganyifu (na kwa kweli maigizo yote ni "uwongo").

Husuda [Zote]: Neno hili pia linaandikwa na Petro katika uwingi (plural), kama

*all's fair in love and war ni methali katika lugha ya Kiingereza.
ilivyokuwa katika neno lililopita, na linasisitizwa na pia linaelekeza fikra zetu katika mifano mahususi ya mwenendo wa husuda na wivu (wakati lingeandikwa katika umoja – singular – lingeweza kutufanya tufikirie kinadharia tu, na ni rahisi kujiona kama vile hatuna hatia ya wivu wa aina yoyote, lakini ni vigumu kufikiria kwamba hatuna hatia ya matendo mengi "madogo-madogo" ya husuda na wivu).

4 Tena nikafikiri amali (kazi) zote, na kila [faida za] kazi ya ustadi, ya kwamba zinatokana na mtu kumwonea wivu/husuda mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha [kukimbilia] upepo [ambao haiwezekani kuuweka kiganjani].
Muhubiri 4:4

4.5  Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu [ameweka] nia Yake dhidi ya wivu wa aina hizo (katika aya za 1-4; rejea pia Wagalatia 5:17)

Kama aya hizi zinavyoweka wazi, husuda/wivu kwa kiasi kikubwa ndiyo dhambi kuu/asilia ambayo kutokana nayo dhambi nyingine nyingi huzaliwa. Katika taswira yake hii, husuda/wivu hufanana na kiburi au majivuno na ufidhuli, lakini yenyewe inadhihirisha uwepo wa majivuno na ufidhuli huo, ukitofautisha na kujiona wenyewe (nafsi) na matakwa yake kuwa ni bora zaidi. Husuda/wivu ni kinyume kabisa cha kukubali kwa amani moyoni mwetu hali ambayo Mungu ametupangia wakati katika ujinga wetu tunajilinganisha sisi katika hali zetu na watu wengine ambao tunawaona kuwa ni bora zaidi – mara nyingi katika mali (ijapokuwa tunapaswa kujua kwamba utajiri wa kiroho ndio muhimu kwetu kuutafuta tukingali hapa duniani, na baraka zote za kidunia zitakuwa mavumbi hivi punde). Kutoridhika na kukosa amani ndiyo matokeo ya kuanguka katika dhambi ya husuda na wivu (Zab. 37:1; Mithali 14:30; 24:1; 24:19; Muhu. 4:8; Matt. 20:15; 1Wakor. 13:4; Wafi. 4:11-12; 1Tim. 6:8; Waebr. 13:5; Yak. 4:2).

5.18  shukuruni kwa [katika mazingira yote] kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
1Wathess. 5:18

2.15  Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba [kwa uhalisia] hakumo ndani yake.
2.16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima [yaani majigambo ya alicho nacho na anayoyafanya], havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
2.17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu [akiwa hai] hata milele.
1Yoh. 2:15-17

Kashfa Zote: Neno la Kiyunani hapa, katalalia, tafsiri sisisi (literal translation) yake ni "sema-chini". Ijapokuwa kitenzi kinachotupa neno hili wakati mwingine kinamaanisha "kusema dhidi ya ...", kuna maana pia ya kumharibia mtu jina au sifa yake kulingana na jinsi Petro anavyolitumia neno hili hapa. Kashfa, kuharibu sifa au jina, kumsemea/kumzungumzia mtu vibaya na/au kueneza tetesi/udaku kuhusu mtu (bila kujali kama habari zinazoenezwa ni za kweli au la), kwa wazi kabisa ni mwenendo usio wa Kikristo [kabisa] (Walawi 19:16; Zab. 15:3; Mithali 10:18; Mrk 7:21-23; 2Wakor. 12:20; Waefe. 4:31):

4.25  Basi uvueni uongo, “mkaseme kweli kila mtu na jirani yake” (Zakaria 8:16); kwa maana [sisi waumini] tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Waefe. 4:25 SUV

4.29  Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Waefe. 4:29 SUV

4.6  Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu (chumvi), mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Wakol. 4:6 SUV

3.1  Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo [wa utawala] na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;
3.2  wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
Tito 3:1-2 SUV

Kwa mara nyingine tena, uwingi (plural) wa neno hili hapa unatumika kwa majumuisho. Petro analitumia namna hii kutusaidia kuona kwamba mambo mengi ambayo sisi wenyewe hatutaweka katika fungu la "kashfa" yanaweza kuwa kiukweli ni kashfa. Kwanza, kwa kuwa sisi si Mungu, dondoo ambazo tunazitolea maoni wakati mwingine si kweli tupu, na karibu wakati wote hazijakamilika. Hivyo, tukiwa na shaka katika jambo, ukimya ni shauri na uamuzi mwema kuliko kutoa hoja hasi kuhusiana na jambo hilo au kumweleza mtu mwingine jambo hilo, haswa akiwa ni Mkristo mwenzetu.

Mtoto Mchanga Anayekua (aya ya 2): Katika aya ya pili, Petro anatumia analojia ya mtoto anayekua kuelezea mchakato halisi wa kukua kiroho kwa Mkristo. Kama vile watoto wachanga wanavyopenda maziwa ya mama ambayo yanawafanya wakue, vivyo hivyo waumini wapya (kwa hakika waumini wote), wanapaswa kupenda "maziwa ya Neno", yaani kweli iliyomo katika Biblia, ili kwamba kwa kujifunza kweli hii nao pia wanakua. Kwa hakika, kukua kwetu si kwa kimwili (ambako kunaonekana kwa macho) bali ni kwa kiroho (ambako hakuonekani kwa macho bali 'kunaonekana' kwa hisia kutokana na matendo na maneno yetu). Tofauti nyingine kati ya mifano hii miwili ni kwamba wakati watoto wachanga wana hulka ya kupenda maziwa ya mama zao na hawawezi kujizuia kuyapenda, waumini wanapaswa kushawishiwa – kama ninavyofanya mimi hapa [kwako] – ili kuchochea kiu ya kupenda maziwa ya kiroho. Hii si kusema kwamba waumini, haswa waumini wapya, hawana hulka ya kuijua kweli – kwa hakika tunayo. Lakini ni kweli pia kwamba kwa kuwa sisi ni wanadamu na tunao utashi [huru], ni rahisi sana kutuondoa kwenye msitari ulionyooka wa kitu tunachojifunza, haswa kikiwa kigumu kidogo na si cha kufurahisha na kuburudisha kimwili na kiakili papo kwa papo (immediately). Bila ubishi wowote kuna kuridhika kwingi na furaha tele katika kuisikia kweli ikifundishwa, kuamini kweli hiyo, na kuitumia kweli hiyo katika maisha yetu. Hata hivyo, inataka juhudi, na furaha na kuridhika ndani ya nafsi zetu [kutokana na kulisikia Neno] kunachukua muda kidogo kutokea, na pia si 'automatic'. Kinachotia faraja sana ni matokeo, lakini matokeo hayo – kupevuka kiroho – hayawezi kuja bila juhudi kubwa, zinazochukuliwa wakati wote, zinazofanyika kwa usahihi, na katika uongofu. Kama vile bila shaka kuna furaha kubwa katika kushinda tuzo ya riadha, ni wazi kabisa kwa wote kwamba matayarisho yake yalihusisha maumivu mengi, kujitoa mhanga na juhudi kubwa – na hayo yote yalipaswa kufanywa katika "namna iliyo sahihi" ili kufanikisha matokeo mazuri. Tofauti na riadha, waumini wote wanaweza "kushinda tuzo" – na kwa hakika hilo ndilo jambo alitakalo Bwana wetu. Lakini kama ilivyo katika riadha, hatuwezi kufikia lengo letu bila bidii na nia madhubuti, za kila siku, kwa muda mrefu na kwa njia sahihi.

2.5  Hata mtu akishindana katika mchezo [wa riadha] hapewi taji, asiposhindana kwa halali [na kufuata sheria].
2Tim. 2:5 SUV

Hii ina maana kwamba ijapokuwa [bila ya shaka] inachukua muda mrefu, juhudi kubwa na matumizi makubwa ya rasilimali ili mtu aweze kuwa mwanachama anayethaminiwa katika 'kanisa' ambamo kweli haifundishwi, juhudi zote hizo na kujitoa kote huko hakuwezi kumfikisha muumini katika kiwango cha kupevuka kiroho, kiwango muhimu ambacho ni lazima kifikiwe ikiwa muumini huyu anataka kuwa na stamina ya kiroho itakayomwezesha kuhimili mitihani ambayo ataikabili katika maendeleo yake ya kiroho katika Bwana ambayo anapaswa kuikabili na kufaulu kabla ya kuingia katika utumishi kwa Bwana. Inahitajika ile kweli ya Biblia kufanikisha hili, kweli iliyomo katika maandiko, iliyoeleweka na kufundishwa kwa usahihi, halafu ikaaminiwa na kutumiwa katika mazingira ya kila siku ya muumini. Wakati mambo mengine yanahitajika ili muumini aendelee na kufikia kiwango cha kupevuka kiroho (kw. mf. sala/maombi, kusoma Biblia, utakaso), hakuna mbadala wa kweli ya Neno la Mungu iliyofundishwa katika uhalisia wake na ukweli . Hayo ndiyo maziwa ya mama yanayotakiwa kwa ajili ya kukua kiroho. Petro, kwa umuhimu mkubwa, anaongeza kwamba "maziwa" tunayohitaji au mafundisho yake ambayo tunayahitaji ni lazima "yasiwe na udanganyifu" au "hila" (neno linalotoka katika mzizi au asili ileile [katika Kiyunani] kama ya neno "hila" tunazoambiwa kuachana nazo katika aya iliyotangulia). Katika jamii zote za Kikristo huko Asia ya wakati huo kama tunavyojua kutokana na maandiko/uandishi wa Paulo na Yohana, wakati wote kulikuwa na tishio lililoelekezwa kwa ile kweli ya Biblia kutoka kwa waalimu wa uwongo wa "rangi" mbalimbali (makundi makuu kati yao wakiwa ni Wanostiki na Judaizers – 'Wakristo' waliofundisha ufuasi wa Sheria ya Musa katika enzi hii ya neema). Ukweli huu wa uwepo wa waalimu wa uwongo kati yetu unasaidia kutukumbusha usemi kwamba "chachu kidogo" hulichachusha donge zima (1Wakor. 5:6; Wagal. 5:9). Kuingizwa kwa mafundisho ya uwongo katika kanuni ambazo vinginevyo zinaonekana kuwa za kweli mara nyingi kunaweza, na huwa, na athari ya kuhujumu imani ya wale wanaosikia mafundisho hayo na kuyafuata. Kama vile tone moja la sumu katika guduria la maziwa linafanya maziwa hayo yawe yasiyofaa kwa matumizi ya mwanadamu, vivyo hivyo tunapaswa kuwa macho na kutahadhari dhidi ya mafundisho yoyote ambayo katika uhalisia wake si ya kweli – haswa kwa vile tunasogea karibu zaidi na zaidi kuelekea mwisho wa dahari ambapo mafundisho ya uwongo ya namna hii yametabiriwa [na Mungu] kwamba litakuwa tatizo kubwa litakalowaletea mauti ya milele watu wengi (cf. Matt. 24:4-5; 24:11; 24:24-27; 2Tim. 3:1-13).

4.1  Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
4.2  wakisema uwongo katika unafiki wao wenyewe, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
1Tim. 4:1-2 SUV

2.1  Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
2.2  Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.
2Pet. 2:1-2 SUV

Hatimaye, katika aya ya pili, Petro anatuambia mahususi kwamba ni katika kunyweshwa maziwa ya Neno la Mungu, yaani kulitafuta kwa kiu, kulisikiliza, na kuliamini, ndipo "tunakua katika wokovu". Hii haina maana ya kwamba hatujaokolewa tayari kama waumini, (tumeshaokolewa), wala haina maana ya kwamba ikiwa tutakuwa bado hapa duniani wakati Bwana wetu anarudi basi hatutaokolewa kwa kufufuliwa pale atakaporudi Bwana wetu katika ule ujio wake wa mara ya pili (tutaokolewa/tutafufuliwa); hii haizungumzii ule wokovu wetu wa mwanzo (positional salvation) {ambao kama waumini, sote tunao}, wala haizungumzii ule usalama kamili wa milele tutakapokuwa salama na Bwana wetu milele (ambao ndio urithi wa wote wanaoamini). Bali kama ilivyo katika utakaso wa katika maisha ya Kikristo hapa duniani (experiential sanctification) {ambao ni tofauti na ule utakaso wa mwanzo (positional sanctification) ambao waumini wote wanao na ule utakaso wa mwisho (ultimate sanctification au utakaso-hitimisho) ambao sote tunaoamini tutakuwa nao katika siku ile ya milele}, wokovu huu unamaanisha matumizi ya hadhi yetu kama waumini kwa ajili ya utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kuongezea kukua kiroho juu ya ule msingi wa imani ambayo sote tunayo (War. 5:9-10; 13:11; 1Wakor. 1:18; 3:15; 5:5; 15:2; 2Wakor. 1:6; 2:15; 1Wathess. 5:8-9; 1Tim. 4:16; 2Tim. 2:10; 3:15; 4:18; Waebr. 1:14; 9:28; Yak. 1:21; 1Pet. 4:18; Yuda 1:23).

2.12  Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyo[i]tii [ile kweli] siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo tu [pamoja nanyi], bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
Wafi. 2:12 SUV

Kuonja ukweli kwamba Bwana ni "Bora Sana" (aya ya 3): Petro anahitimisha mlinganisho wake kati ya muumini anayekua na mtoto anayekua kwa kutumia msisitizo wa nakshi/pambo la kifasihi (lugha), akitumia kile kinachoitwa katika sarufi ya Kiyunani "a simple condition" ambayo kwa kweli maana yake si rahisi hata kidogo! Kama ilivyotafsiriwa hapo juu, mbinu hii ni sawasawa na kishazi sababishi (causal clause), lakini kimefanywa kinyume ili kuleta kishindo cha drama kwa kiasi fulani. Waumini waliofanya maendeleo japo kidogo katika maisha yao ya Kikristo kwa hakika wanapaswa kujua kwamba Bwana ni "bora sana". Neno la Kiyunani chrestos lililotumika hapa ambalo tunalitafsiri [kama] "bora sana" – excellent – si neno la kawaida sana kulitumia katika kutafsiri wema, na mara nyingi linatumika kuleta maana ya -enye kufaa, -enye uhodari, na -enye manufaa. Hivyo, wakati "mkarimu", "mwadilifu", "wa kufurahisha" na "mwema" yote yanakubalika kama tafsiri ya neno chrestos kama Petro anavyolitumia hapa, "bora sana" – excellent – inaleta maana ya, kwanza, utimilifu wa hulka ya Bwana wetu, na pili, usimamizi Wake ulio mtimilifu wa maendeleo yetu ya kiroho – ambayo ndiyo dondoo kuu ya Petro hapa. Kwa hakika tunapaswa kuwa na kiu ya maziwa ya Neno la Mungu na kwa hakika tunapaswa kujizatiti katika jukumu la kujikuza kiroho. Kwani "tulionja" wema Wake na ubora Wake wa kiwango cha juu pale tulipookolewa kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kila kitu tulichopitia tangu hapo kwa jinsi tulivyojifunza juu Yake na tulivyoanza na kuendelea kutembea kwa ukaribu zaidi na Yeye siku hadi siku kimetuhakikishia wema huo, ubora huo mkuu, manufaa katika maendeleo yetu yote ya kiroho: si kwamba Petro anatuambia kitu chochote ambacho hatukijui au ambacho hatupaswi kukijua tayari na ambacho hatupaswi kuwa tunakifanyia kazi tayari katika maisha yetu, kwani kwa kuwa sasa tumekula kutoka katika mti halisi wa uzima, tunajua kabisa "utamu" wa ile kweli, na jinsi ilivyo bora kabisa katika uwezo wake wa kutuleta hatua kwa hatua karibu na Bwana wetu Yesu Kristo ili tuzidi kumfurahisha siku hadi siku, vile tunavyopaswa kufanya (Zab. 119:103; Waebr. 6:4-5).

8 Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
Zab. 34:8 SUV

Kristo Jiwe Lililo Hai (aya ya 4): Bwana Yesu Kristo ndiye Jiwe/Mwamba (Kumb. 3:4; 1Sam. 2:2; 2Sam. 22:47; Zab. 18:2; 18:46; 19:14; 61:2; 118:22; 144:1; Isa. 17:10; 28:16; 44:8; 51:1; Hab. 1:12; War. 9:33; 1Wakor. 10:4; cf. Kut. 17:6; Hes. 20:8; Kumb. 32:4-37; Isa. 8:14-15), Jiwe la msingi la Kanisa (Matt. 16:18; 1Pet. 2:6), "Jiwe lenye uhai" ambalo kwalo "tumekuja" (1Pet. 2:4), na Ndiye msingi wa "mjengo" wetu wote wa kiroho (Matt. 7:24-25; Lk. 6:47-49; 1Wakor. 3:11). Taswira hii ya shani ya Kristo inatuonyesha mara moja uaminifu Wake na utumainifu Wake, na wakati huo huo ikidhihirisha waziwazi kwamba tunamhitaji Yeye kabisa kabisa na tunapaswa kuweka imani yetu Kwake: kama vile jengo linavyolazimika kusimama juu ya msingi imara, vivyo hivyo hatuwezi kuokolewa na hatuwezi kufanya maendeleo ya kiroho bila ya kumtegemea Yeye kwa asilimia 100, kwani Yeye ndiye msingi wa imani yetu, wakati tunaokolewa na pia wakati wote unaofuata katika kila hatua tunayopiga mbele katika kumfuata Yeye. Hivyo, wakati "Jiwe" au "Mwamba" ni jina timilifu la heshima kwa ajili ya Mwokozi wetu mtimilifu asiyebadilika, linapaswa kuweka akilini mwetu uhusiano wetu wa moyoni kabisa na Yeye anayeaminika kwa asilimia 100: Bwana Yesu Kristo ndiye Mwamba wa mambo yote katika maisha yetu kama Wakristo hivyo kwamba tunakuwa salama na thabiti hata yakija mafuriko ya aina gani ikiwa tu tunaendelea kumtegemea Yeye.

Lililokataliwa na wanadamu, bali katika macho ya Mungu [Baba] ni teule, lenye heshima kuu (aya ya 4): Tunaambiwa katika 1Wakor. 2:8 kwamba kama watawala wa dunia hii wangelijua Kristo ni nani haswa – mteule na anayeheshimiwa kwa ukuu na Baba Mwenyewe – wasingemsulibisha. Na kama ambavyo alikuwa, na anaendelea, kudharauliwa na dunia – bali si na Baba yake ambaye ni Baba yetu pia – vivyo hivyo sisi tulioamua kukaa upande wake Yeye aliyeamua kuwa na sisi, tunadharauliwa na kubezwa na dunia. Lakini kama vile alivyopewa heshima ya juu kabisa, yaani Jina lililo juu ya majina yote ambalo mbele Yake kila goti litapigwa (Wafi. 2:9-11; cf. Waefe. 1:21), vivyo hivyo nasi tunaostahamili katika Yeye tutatukuzwa pamoja Naye katika siku ile kuu na tukufu inayokuja (War. 8:17; 8:30; 2Tim. 2:10). Sisi pia ni wateule katika Yeye aliyeteuliwa, tuliochaguliwa mahususi kuwa sehemu ya Mke wa Bwana Yesu kama ilivyoagizwa katika mpango wa Baba tangu milele iliyopita (War. 8:29-30; 8:33; 11:7; Wakol. 3:12; 2Tim. 2:10; Tito 1:1; 1Pet. 1:2). Ulimwengu una vipaumbele vyake na mfumo wa ngazi za maadili yake. Lakini yote hayo hayana maana kwetu. Tumaini letu lililobarikiwa ni la ufufuo na uzima wa milele, na thawabu njema kutoka Kwake Yeye tuliyemchagua badala ya ulimwengu.

15.18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
15.19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
15.20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
Yoh. 15:18-20 (cf. Matt. 10:25; 1Yoh. 3:13)

3.10  Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
3.11  Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
3.12  Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri [itakapopimwa ubora wake].
3.13  Maana siku ile [ya hukumu] itaidhihirisha [jinsi ilivyo kiuhalisia], kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu [utaipima] kazi ya kila mtu, [ina ubora wa] namna gani.
3.14  Kazi ya mtu aliyoijenga juu [ya imani] yake [katika Kristo ikipona tathmini ya moto], atapata thawabu [kwa kazi hiyo].
3.15  Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara [ya kutothawabiwa]; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa [kupitia katikati ya] moto [ambao ulitathmini kazi yake na kuiona haina thamani na kuiunguza].
1Wakor. 3:10-15

Mawe Yenye Uzima yanayojengwa na kuwa Nyumba ya Kiroho (aya ya 5): Kama tunavyosimuliwa katika Mathayo 16:18 ambapo Bwana wetu alimpatia Petro jina lingine na akamwita "jiwe" (petros) kuonyesha kwamba Petro atakuwa sehemu muhimu sana ya lile "fumbo" kuu la upanuzi wa Kanisa utakaojengwa (uliojengwa) juu ya "Jiwe Kuu" (petra), "Mwamba" ambao si mwingine bali ni Kristo Mwenyewe, Msingi, Jiwe la Msingi na Kichwa cha Kanisa – vivyo hivyo Petro anatuelezea sisi kuwa ni "mawe", sehemu zinazofanana za mjengo wa milele ambao Bwana Yesu Kristo anaujenga, "mawe yenye uhai", kwa sababu Kanisa si mjengo wa matofali na saruji visivyokuwa na uhai, bali ni mkusanyiko hai wa watu waaminio ambao wanaishi kiroho, waliojengwa muumini mmoaja baada ya mwingine, kutoka Adamu na Eva mpaka sasa na baadaye litakapohitimishwa katika siku ya kurudi kwake Yeye akiyejaa utukufu mkuu. Analojia hii nzuri aliyopewa Petro na Roho Mtakatifu, kwa wakati mmoja inaelezea umoja wetu kila muumini na mwenzake, na pia jukumu la kusisimua ambalo sisi sote tunashiriki. Sisi sote ni mawe katika jengo, yaliyo hai katika jengo lililo hai ambalo msingi wake ni Bwana wa uzima aliyetupatia uzima wa milele na ambaye ametufanya wamoja na Yeye, na kila mmoja na mwenzake. Na jukumu hili halijakamilika bado, na halitakamilika mpaka ile siku ya ufunuo Wake na ambayo itakuwa siku ya mabadiliko yetu katika ufufuo, atakapokuja mara ya pili. Lakini kumalizika kwa mjengo huu wenye uhai ambamo sisi sote tunaoamini tutashiriki milele, tukijumuisha kaka na dada zetu wote katika Kristo na msingi wake ukiwa Kristo Mwenyewe (Mwamba [M]wenyewe) ambaye ndani Yake tumeweka imani kwa ajili ya uzima wa milele, ni kwa uhakika kabisa. Yawezekana mtu mmoja mmoja kushindwa (Lk 14:28-30), lakini pamoja sote kama Kanisa, washiriki wa Kristo kila mmoja wetu (Yoh. 17:11; 17:20-23; 1Wakor. 1:10; Waefe. 4:3-13), tutasonga mbele na kushinda dhidi ya upinzani wote kutoka kwa yule mwovu mpaka tutakapokamilika katika Kristo kwa namna zote katika ile siku, "na hata malango ya kuzimu (hell)" yenyewe hayataweza kutuzuia au kutushinda katika hili jukumu takatifu (Matt. 16:18).

2.19  Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapita njia, bali ninyi ni wenyeji [raia] pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
2.20  Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
2.21  Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
2.22  Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika [uweza wa ] Roho [Mtakatifu].
Waefe. 2:19-22 SUV

3.6  bali Kristo [Alikuwa mwaminifu], kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; Ambaye nyumba yake ni sisi, ikiwa kwa kweli tutalishika lile tumaini [ambalo kwalo] tunasikia fahari iliyo imara mpaka mwisho.
Waebr. 3:6

Makuhani Watakatifu kwa ajili ya kutoa Dhabihu za Kiroho (aya ya 5): Ijapokuwa twaweza kuwa watu wa mataifa, ijapokuwa binafsi twaweza kuwa si kizazi cha Walawi, na ijapokuwa wengi wetu ni wanawake na si wanaume, waumini wote katika Bwana Yesu Kristo ni makuhani wa Mungu, kama aya hii inavyotuhakikishia. Kwa hakika hili linaleta maana kwani Kristo Mwenyewe ndiye Kuhani Mkuu wa mwisho (1Tim. 2:5; Waebr. 7:24-25; cf. Ayubu 16:20-21; Isa. 53:12b; Waebr. 6:19-20; 9:11-12; 9:24), na sisi ni wamoja pamoja Naye (Yoh. 14:20; 15:1ff; War. 16:7; 2Wakor. 5:17; Waefe. 2:6; 2:10; Waebr. 3:14; 1Pet. 5:14; cf. Matt. 28:18-20; Waefe. 3:6; Waebr. 3:1; 3:14; 2Pet. 1:4).

2.17  Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya[nayohusiana na] Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake [kwa dhabihu Yake Mwenyewe].
Waebr. 2:17 SUV

Kwa hiyo, ndugu, [kama mlivyo sasa] mliotakaswa na washiriki wa mwito kutoka mbinguni, wekeni mioyo yenu katika Yeye tunayemkiri kuwa alitumwa kuja [kutuokoa] na ambaye ndiye Kuhani Mkuu [wa wokovu huo] Yesu Kristo.
Waebr. 3:1

Basi, kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu aliyepita mbingu zote (yaani kama apitaye katikati ya pazia la hekalu), yaani Yesu, Mwana wa Mungu, na tushike imara tamko letu [la imani katika Yeye]
Kwani Yeye ni Kuhani Mkuu mwenye kuyaelewa na kuwa na rehema kuu juu ya madhaifu yetu, kwa kuwa hata Yeye alipitia mitihani katika yote ambayo sisi tunapitia, bali bila ya kutenda dhambi.
Waebr. 4:14-15

Na ametufanya [sisi] kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba Yake – utukufu na ukuu u na Yeye hata milele na milele. Amina.
Ufu. 1:6
AU:
1.6  na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.
Ufu. 1:6 SUV

5.9  Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
5.10  ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki [watatawala] juu ya nchi.
Ufu. 5:9-10 SUV

Dhabihu za Kiroho (aya ya 5): Ni muhimu kusisitiza kwamba huu ukuhani mpya ambao waumini wote katika Kristo ni sehemu yake una tofauti kubwa na ule wa Walawi – kama vile Ukuhani Mkuu wa Kristo ulivyo bora zaidi ya ule wa Walawi (Waebr. 7:1-28). Kristo ni Mfalme wa wafalme na pia ni Kuhani wa makuhani, akijumuisha mamlaka yote mawili katika nafsi moja (Zab. 110:1-4; Zakaria 6:13b; Waebr. 7:1; cf. Jer. 33:16-18). Hivyo kama nukuu hizo mbili hapo juu zinavyodhihirisha, siyo tu kwamba ukuhani ambao sisi waumini tunashiriki unatofautiana na ule wa Ki-lawi kwa sababu tumepewa huo kwa msingi wa uhusiano wetu na Kristo, Yeye aliye Kuhani Mkuu, bali ukuhani huu umeungwa imara na hauwezi kuachanishwa na utawala tutakaoshiriki Naye, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana (War. 8:17; 2Tim. 2:12; Ufu. 1:6; 2:26-27; 3:21). Kwa hivyo, dhabihu tunazotakiwa kuzifanya nazo zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na zile dhabihu za Ki-lawi kwani kwa hulka yake ya sasa hizi ni za kiroho tu na hivyo ni halisi, zikichukua nafasi ya zile za zamani ambazo zilikuwa ni ishara katika Sheria ya Musa (1Wakor. 5:7; Wafi. 2:17; 4:18; Waebr. 13:15) – hizi ndizo "dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu" ambazo Petro anazizungumzia katika muktadha wetu hapa.

12.1  Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, [hii] ndiyo ibada yenu [kama makuhani] yenye [kumfurahisha Mungu, mnayoifanya kiroho].
12.2  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua [kwa] uhakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
War. 12:1-2 SUV

Na kuwa wamoja na Kristo na makuhani pamoja Naye, badala ya kuhitaji msuluhishi wa kutuwezesha kukisogelea kile kiti cha enzi cha neema katika sala, sasa tunafaudu ufikikaji (access) wa moja kwa moja na wa mara moja [unapohitajika] kwa Mungu Baba (Waefe. 2:18; 3:12; cf. Yoh. 14:13-14; War. 5:1-2).

4.16  Basi na tukikaribie kiti cha neema [cha Baba] kwa ujasiri, ili tupewe rehema [Yake], na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebr. 4:16 SUV

Kuhusu hizi "dhabihu za kiroho", kama vile makuhani wa Ki-lawi walivyoendesha ibada kama ilivyotakiwa na Sheria ya Musa kutokana na matakwa ya maandiko, vivyo hivyo kila muumini leo hii [au enzi hii] amepewa angalau kipaji kimoja (karama) cha kiroho na Roho Mtakatifu, na amepewa utumishi wa aina yake na Bwana Yesu Kristo, na matokeo yake yamepangwa na Mungu Baba [kabla ya kuumbwa ulimwengu] (1Wakor. 12:4-7). Tunapaswa kujizuia sana kuzichukulia huduma (utumishi wetu) katika maana ambayo(zo) madhehebu mbalimbali (the church-visible) yamelitumia neno utumishi (ministry). Utumishi wa aina zote ambao kikweli umeamriwa na Kristo utapelekea katika mchango wa aina fulani katika kukua kiroho kwa Wakristo wengine, iwe moja kwa moja au vinginevyo. Hivyo, ikiwa muumini anafundisha Neno la Mungu au anasaidia kwa namna fulani katika huduma ya mafundisho, ikiwa binafsi anajihusisha na uinjilisti, au anawasaidia wale ambao wanawatia moyo watu kumtafuta na kumfuata Kristo au wanafanya hivyo kwa namna fulani isiyo ya moja kwa moja, utumishi wote wa kweli siku zote utaendelea na kueneza ukweli wa Neno la Mungu, kwa sababu ni kwa njia ya kweli inayotiwa nguvu na Roho Mtakatifu pekee ndiyo tunaweza kuwa na tumaini la kujua utumishi ambao Bwana wetu ametupangia.

12.1  Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, [hii] ndiyo ibada yenu [kama makuhani] yenye [kumfurahisha Mungu, mnayoifanya kiroho].
12.2  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua [kwa] uhakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
War. 12:1-2 SUV

Ndiyo maana imeandikwa (aya ya 6): Usemi wa Petro unaotangulia nukuu inayofuata (kutoka Isaya 28:16) unadhihirisha kwamba Isaya alipozungumzia Mwamba wa Sayuni alikuwa anamaanisha Masihi, akimtazamia Kristo katika siku za usoni (kwa wakati ule) ambaye ndiye Mwamba ambao juu Yake imani yetu kila mmoja ina msingi wake na inasimama imara. Yeye ndiye Jiwe la pembeni kwa ajili ya mjengo ambao sisi sote ni sehemu yake [mjengo huo]. Yeye ndiye Jiwe la msingi ambalo limechaguliwa mahususi, nasi ndani Yake tumeteuliwa. Yeye ndiye Jiwe la kito cha thamani kisichokuwa na bei [ya kidunia] mwenye thamani kuu kwa Baba [na] ambaye kupitia Kwake tunachukuliwa [sasa] na Baba kuwa ni wapendwa. Na tunao uhusiano huu Naye, ambao ndio msingi wa kila kitu katika Kanisa, kupitia au kutokana na imani yetu Kwake. Kwa imani yetu ndani Yake, 'hatutaingia katika aibu', kama Petro anavyotohoa (adapt), akiongozwa na Roho Mtakatifu, andiko la Isaya anaposema kwamba "kamwe hatutatingishwa".2 Tunapoliona hili kwa mtazamo wa wanadamu wanaomwamini Kristo, kwa kuweka imani yetu katika Yeye hatuna cha kuogopa kuhusiana na uzima wetu wa milele ijayo; tunapoliona hili kwa mtazamo wa analojia ya mjengo, sisi tulio mawe [ya mjengo huo] yanayoishi, hatutang'olewa kutoka katika nafasi yetu katika jengo hili timilifu, Kanisa, ambamo tumewekwa kwa mpango timilifu na mjenzi Mtimilifu, Baba yetu wa mbinguni, wakati mjengo wote ukisimama imara juu ya msingi mmoja, Bwana wetu Yesu Kristo. Hivyo kwa kufanya unabii wa ujio [wa kwanza] wa Mwamba na umoja wetu wa karibu Naye, Isaya pia kwa maneno mengine alitabiri ushiriki wetu katika yote aliyo nayo Masihi na yote yaliyo (is) Masihi, pamoja na ufalme Wake na ukuhani Wake – "hii ndiyo sababu ya nukuu hii ya Petro katika maandiko".

Heshima hii (aya ya 7): Kufikika moja kwa moja kwa Baba tunakofaudu kutokana na muungano/umoja wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo ni hali ambayo haikuwepo katika enzi mbili zilizopita: ile ya kwanza ya Mataifa (Gentile Age) – Adamu hadi Abrahamu, na ile ya pili ya Wayahudi (Jewish Age) – Abrahamu hadi Bwana Yesu, kila [enzi] moja ikiwa na/ya miaka elfu mbili, na ni heshima ya kipekee kweli.* Kwa kuwa hatuwezi kuiona wala kuihisi hali hii, ya kufikika moja kwa moja kwa Mungu Baba yetu, tunaweza kuelewa, ijapokuwa ni kwa masikitiko kidogo, kwamba labda hatuitambui kwa undani hadhi hii kubwa tuliyo nayo katika Bwana Yesu Kristo ya kuwa makuhani wa kifalme wa Mungu kwani tunashiriki katika kila kitu ambacho Bwana wetu amekipata kama nyara kutokana na ushindi Wake pale msalabani.

* Kwa sasa tuko katika enzi ya Kanisa (Church Age) – tangu ufufuo wa Kristo mpaka mwisho wa Dhiki Kuu, katika Ujio wa Pili wa Kristo. Enzi ya Kanisa nayo ni ya miaka 2000 pia.
Inatupasa sisi kama waumini tukumbuke, angalau mara moja moja, neema nyingi kuu tulizo nazo kama sehemu ya Mke na Mwili wa Kristo, haswa katika nyakati ambazo tutapungukiwa na ile furaha katika Bwana ambayo tunapaswa kuwa nayo wakati wote na ambayo ndiyo chemchemu (chanzo) yetu ya kweli ya nguvu zetu (Neh. 8:10).3 Ulimwengu hauwezi kuona na kwa hakika hautambui ukweli kwamba
Wakristo, hata wale walio katika hali za kiuchumi za chini kabisa katika dunia hii, wamepewa heshima kuu na Mungu na kupewa hadhi ambayo inazidi uwezo wa walio wakuu kuliko wote wa dunia hii. Waovu wa hapa duniani wanaweza kutukebehi, lakini Mungu anawakebehi wao (Zab. 37:13),nasi tuna haki zote za kufurahi na nafasi ya kufika moja kwa moja kwenye kiti cha enzi cha Mungu Baba tuliyo nayo. Kwani tunajua kwamba hadhi hii ni halisi na ya shani kupita maelezo – kwa imani.

4.18  tusiviangalie [na kuvitegemea] vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
2Wakor. 4:18 SUV

5.7  Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.
2Wakor. 5:7 SUV

11.1  Basi imani [katika Neno lililoandikwa na lenye uhai] ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, [imani] ni bayana [proof] ya mambo yasiyoonekana.
Waebr. 11:1 SUV

Lakini kwa wale wasiotii (aya ya 7-8): Kuwa kuhani wa kifalme wa Mungu Baba kwa msingi wa kushiriki katika ukuhani wa Kuhani Mkuu Bwana Yesu Kristo ni heshima kuu kweli kweli, na tofauti kati ya hadhi ya nafasi yetu katika Kristo na ile ya asiyeamini ni kubwa isivyomithilika. Kwani hata kama ilivyokuwa kwa Lazaro masikini, ambaye hali yake ya hapa duniani ilikuwa duni kabisa ikilinganishwa na ya yule tajiri ambaye Lazaro alikuwa akilala getini kwake, tunajikuta katikati ya dhiki na mitihani ya moto [mkali kweli] hapa duniani (na hili ni jambo linalowakuta Wakristo wote halisi: 2Tim. 3:12), tunajua fika kwamba neema za muda za wale wanaokataa kumpokea Kristo ni za muda kweli kweli. Kwao, Kristo ni jiwe ambalo kwalo wanajikwaa. Maana yake ni kwamba Bwana Yesu ndiye suala katika maisha ya kila mmoja, na kwamba wote wanaokataa kumkubali Yeye wanadhihirisha tu kwa kumkataa kwao huko, iwe kukataa kwa tamko na matendo waziwazi au kukataa kwa kusema wazi wazi au kukataa kwa kutosema na kutofanya chochote juu Yake, kwamba hawana kiu ya kuishi milele na Mungu. Hivyo Bwana Yesu Kristo na kile ambacho kila mmoja wetu anakifikiria na kuamua juu Yake ndilo suala muhimu kuliko yote. Wajenzi (yaani viongozi wa Wayahudi wa wakati ule) walimkataa Yeye ambaye kwa hakika ndiye Jiwe la Pembeni, msingi ambao juu yake uumbaji umefanyika – kwani msalaba ndio moyo wa mpango wa Mungu alioufanya hata kabla ya uumbaji. Lakini katika siku ile kuu inayokuja, ukweli kwamba Bwana Yesu ndiye Alpha na ndiye Omega hautaweza kupingwa na hivyo mbele Yake "kila goti litapigwa" (Wafi. 3:10; cf. Isa. 45:23; War. 14:11) na kukubali kwamba Yeye ndiye Bwana wa wote na vyote. Kwa hatma hii "waliteuliwa" katika mpango wa Mungu, lakini hili halina maana ya kwamba hakukuwa na utashi huru uliofanya maamuzi kwa upande wao. Kwani ni kwa kuwa "walidhamiria kutokuwa watiifu kwa lile Neno" (1Pet. 2:8), yaani kwa Injili ambayo inafunua kwamba wokovu unapatikana kwa njia ya imani katika Kristo pekee, na ndipo wasioamini wanajikwaa, kwa kosa lao wenyewe, kwa kukataa ile kweli, wao wenyewe. Katika haki Yake kuu, Mungu Baba anawapa wasioamini haki/uwezo wa kufanya uamuzi kuhusu hili, na uamuzi huu [umeandikwa na kuamriwa] katika mpango na maagizo ya Mungu.

Jamii Teule (aya ya 9): Baada ya kuielezea hali mbaya, ya kujitakia, ya wale wasioamini, na baada ya kutukumbusha majukumu yetu kuhusiana na utakaso kabla ya hapo, Petro anaweka kituo kidogo hapa ili atutie moyo kwa kutukumbusha juu ya hadhi kuu ya ajabu iliyo vigumu kueleza ambayo tunayo kama waumini wa Bwana Yesu Kristo. Hili ni somo jema kwa yeyote anayefundisha au anayeshuhudia Neno la Mungu kwa watu wengine. Mbadala wa kuamini (yaani kutoamini) ni wa kutisha sana (matokeo yake), hii ni kweli, na majukumu ya muumini ni mengi na makubwa, hii ni kweli pia, lakini neema zinazotokana na kuwa na Bwana Yesu Kristo na kuwa na Mwana wa kweli wa Mungu ni lilizotukuka kweli kweli na kwa kweli "mzigo" wa kuwa Mkristo ni kitu kidogo sana ukilinganisha na faida zake. Kuwa na mtazamo uliosawazika katika kuielezea ile kweli ni jambo muhimu sana. Kila mara unaposhuhudia Injili unapaswa kuuelezea uhalisia wa pande zote mbili – neema zinazotokana na wokovu na maafa yanayotokana na kumkana Kristo. Na kila mafundisho ya ile kweli ya maandiko vivyo hivyo yanapaswa kuwa na mchanganyiko uliopimwa kwa busara wa neema na thawabu tunazoahidiwa kama waumini wa Kristo tuliojiwajibisha wenyewe katika kumfuata Yeye pamoja na changamoto, wajibu na majukumu tuliyo nayo yanayotokana na kumfuata Yeye. Hicho ndicho Petro anakifanya katika mifano yote miwili katika sentensi iliyopita, akichukua muda kidogo kuwatia moyo wasomaji wake kwa kuwakumbusha wasomaji wake kuhusu hadhi yao ya juu kama Wakristo na kisha anaendelea kwa kuwasihi kuhusu matumizi sahihi ya kweli wanayojifunza kutoka katika maandiko hapa duniani (katika aya ya 11 na zile aya zinazofuata).

Kutokana na tafsiri ya maandiko inayoitwa Septuagint (LXX Codex) katika sura na aya 43:20 ya kitabu cha Isaya (ambapo maneno ya Kiyunani yanayotumika ni yale yale), tunaweza kusema ya kwamba msemo "jamii/mbari teule" unatumiwa na Petro kuelezea/kumaanisha cheo cha Kiebrania "watu wateule" kinachoonekana katika aya hii (tizama pia matumizi yanayofanana katika Kumb. 7:6; 10:15; 1Mambo ya Nyakati 16:13; Zab. 105:6; Isa. 45:4; 65:9; 65:15; 65:22; cf. War. 9:11; 11:5; 11:7; 11:28). Tunapowajadili wengine ambao kwa namna hiyo hiyo "walichaguliwa" na Bwana, kwa mfano Masihi (Isa. 42:1; Yoh. 1:34; 1Pet. 2:4; 2:6; cf. Lk 23:35), Daudi (Zab. 89:3) na Musa (Zab. 106:23), tunaweza kusema kwamba kuwa pamoja na WAKUU HAO ni jambo jema kabisa. Tunaweza kusema pia kuwa "kuchaguliwa huku" katika Isaya 43:3 (na aya zinazofanana nayo) kunazungumzia waumini katika Israeli kama inavyowezekana kufasiriwa kutokana na ukweli kwamba Musa na Daudi – na kwa hakika Masihi – "hawakuchaguliwa" kwa sababu ya "damu" au utaifa wao tu, bali kwanza kabisa kwa sababu za kiroho. Hivyo ijapokuwa mwanzoni inaweza kuonekana kama vile ni ajabu/kitu cha kushangaza kwa Petro kuonekana kuwa anasema kuwa watu wa mataifa (ambao ndio aliowaandikia waraka huu) ndio walengwa wa neema hii ambayo hapo mwanzo ilieleweka kuwa ni ya Israeli pekee, anatuambia hapa moja kwa moja kwamba kwa njia ya imani yetu kwa Kristo kwa neema ya Mungu nasi pia (watu wa mataifa – Gentiles) ni wanufaishwa wa uteule huo huo, tukifanywa sehemu ya watu na familia ya Mungu, kama ilivyokuwa kwa Waisraeli wa kale na wa sasa – wale wanaoamini tu, kwani bila imani haiwezekani kumfurahisha Mungu wala kufaidika na fadhila zozote [za milele] kutoka Kwake (Waebr. 11:6). Sisi watu wa mataifa ni kama tawi la mzeituni wa porini, lakini tumepandikizwa katika mti wa mzeituni wa Israeli na tunafaudu neema zile zile kutokana na nafasi yetu katika Kristo: sote ni sehemu ya "wateuliwa" wa Mungu katika Kristo.4 Hivyo, wakati sisi ni "wateule" kwa maana ya kwamba Mungu ametuchagua ili tuokolewe kila mmoja wetu katika Mpango Wake [hata] kabla ya historia kuanza, yaani kabla ya kuumbwa ulimwengu (kama Petro anavyoelezea pale mwanzo wa waraka huu: 1Pet. 1:1-2; cf. 1Wathess. 1:4), nasi pia tumekuwa sehemu ya "wateule Wake", yaani Mke na Mwili wa Kristo, Kanisa, ambalo linajengwa juu ya msingi wa Israeli (Waefe. 2:20).

Uteule: Katika kanuni/mafundisho ya Kikristo/Biblia, "uteule" unaonekana kwa ujumla kuwa ni suala la mtu mmoja, suala la Mkristo. Hata hivyo, kama mjadala wa hapo juu unavyoweka wazi, tendo la "kuchagua" (ambalo ndilo linatupa dhana ya uteule au uchaguzi) ni la/linafanywa na Mungu, na uteule huu katika Agano la Kale ulielekezwa kwa taifa moja, uzao wa Abrahamu, watu wa Kiyahudi wa Israeli. Kwa uhakika tunajua kutokana na ufunuo wa aya lukuki katika Agano Jipya (pamoja na la Kale) kwamba kwa kweli wanaoamini tu ndio wanaookolewa bila kujali asili yao (hivyo kwamba kwa maana hii "sio wote ni Israeli walio uzao wa Israeli": War. 9:6). Na twaweza kusema kwa kujiamini kwamba waumini wote katika historia yote, wameokolewa, hata kama muumini fulani kati yao hakuwa na neema ya kuwa uzao wa Kiyahudi (kw. mf. Waefe. 2:8-9). Hivyo basi, sehemu zote mbili za kauli hii ni muhimu kuziweka akilini. Mungu aliwachagua watu wa mbari (race) fulani kuwa mali Yake pekee, na wakati huo huo sisi watu wa mataifa tumepewa neema ya kuingizwa katika ushirika huo kwa dhabihu ya Bwana Yesu Kristo na imani yetu katika kile alichokifanya kwa faida/ajili yetu:

2.11 Hivyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa mataifa, mkiitwa "wale wasiotahiriwa" na wale walio uzao wa tohara ya kimwili na iliyofanywa na wanadamu.
2.12 Kumbukeni kwamba mlikuwa bila Kristo, mliotengwa na dola ya Israeli, msioshirikishwa katika maagano [yake] ya ahadi, bila matumaini na bila Mungu hapa duniani.
2.13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi ambao mlikuwa mbali kabisa mmeletwa karibu kwa damu ya Kristo.
2.14 Kwa maana Yeye mwenyewe ndiye amani yetu, kwani amewafanya wote [Wayahudi na watu wa mataifa] kuwa wamoja, na ameuvunja ukuta wa utengano, yaani ule uadui kati yetu,
2.15 kwa kuziondoa katika Sheria amri na masharti yake [amri hizo] kwa njia ya mwili Wake, ili aweze kuyaumba upya hayo makundi mawili (i.e. aya ya 11) ili yawe Mtu mmoja mpya kwa kusimika amani hii kati yao,
2.16 na kuyapatanisha yote [yakiwa] katika mwili mmoja , na Mungu, kwa njia ya msalaba Wake, baada ya kuitumia njia hiyo [ya msalaba] kumaliza uadui [kati ya Mungu na wanadamu].
2.17 Kwani alipokuja [mara ya kwanza], alitangaza Injili ya amani kwenu ninyi mliokuwa mbali sana [na Mungu], na [alitangaza] amani kwa wale waliokuwa karibu (Isa. 57:19).
2.18 Kwa maana ni kwa Yeye sisi sote tumemkaribia Baba katika Roho.
2.19  Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapita njia, bali ninyi ni raia pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
2.20  Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni Jiwe kuu la pembeni.
2.21  Katika Yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
2.22  Katika Yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu kwa Roho.
Waefe. 2:11-22

Msingi wetu wa kuchaguliwa na Mungu ni imani yetu; matokeo ya kuchaguliwa na Mungu ni umoja wetu katika Mwili mmoja, Kanisa, ambalo ndilo "Israeli ya Mungu" (Waga. 6:16); na njia ya kufanikisha uchaguzi huu ni dhabihu ya Bwana Yesu Kristo, na bila ya dhabihu hii hakuna mpango wa Mungu. Dhabihu ya Kristo ndiyo mpango wa Mungu. Hizi ndizo dhana/dondoo muhimu za kuweka akilini pale tunapoitafakari kanuni ya uteule. Baadhi ya walimu wa teolojia wanasisitiza uchaguzi wetu na Mungu kama Mkristo mmoja mmoja kama ni suala lililo mbalimbali na:

1) utashi wetu huru kama sehemu muhimu ya mlinganyo huo,
2) lengo na matokeo ya uteule huu kuwa ni kuingizwa kwetu katika ushirika mmoja wa Israeli halisi, Kanisa la Bwana Yesu Kristo,
3) msalaba ambao ndio unaweka uwezekano wa uteule wetu.

24.22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Matt. 24:22 SUV

24.24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Matt. 24:24 SUV

24.31 Naye atawatuma malaika zake pamoja kwa sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule Wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Matt. 24:31 SUV

18.7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku; [je, Atachelewa katika hili]?
Luka 18:7

8.33  Ni nani atakaye[thubutu ku]washitaki wateule wa Mungu? [Kwani] Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
War. 8:33 SUV

1.3  Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa neema zote za kiroho, [zilizo] katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
1.4  kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Waefe. 1:3-4 SUV

3.12  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Wakol. 3:12 SUV

1.4  Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;
1Wathess. 1:4 SUV

1.10  Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo [maadili, kukua kiroho na kuzaa matunda] hamtajikwaa kamwe.
2Pet. 1:10 SUV

17.14  Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Ufu. 17:14 SUV

Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika tafsiri tunazosoma za Kiswahili (hata za Kiingereza), hakuna mkanganyiko katika kikundi cha maneno kinachotokana na tafsiri ya Kiyunani ya maneno "wateule" na "uteule". Kwa mfano, maneno haya yanaweza kuchanganywa na maneno "uchaguzi" na "waliochaguliwa" katika tafsiri [kadhaa] za Biblia [za Kiingereza] ambazo mahala pengine linatumika neno "wateule", kutokana na neno lile lile [la Kiyunani]! Hii inakuwa si tatizo ikiwa msomaji anafahamu/anaelewa kwamba uteule ni uchaguzi wetu unaofanywa na Mungu Baba katika Bwana Yesu Kristo, na kwamba tunachaguliwa kwa sababu ya imani yetu katika Bwana Yesu Kristo, na hili limewezekana tu kwa sababu Yeye ametugomboa kwa damu Yake, kifo chake cha kiroho msalabani ambapo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu zote. Wote wanaoitikia wito wa Mungu kwa njia ya imani katika Injili ya Bwana Yesu Kristo wanateuliwa (Matt. 20:16; 22:14; 2Pet. 1:10; Ufu. 17:14; cf. War. 8:29-30). Uteule unathibitisha hadhi hii yetu kuwa ni wale walio wa familia ya Mungu milele katika Bwana Yesu Kristo, na kanuni hii inafundisha ushiriki wetu katika ufalme ambao tunautazamia kwa shauku kuu. Kitu muhimu katika maisha yetu siyo kile kinachopendwa na ulimwengu – kwani ulimwengu huu unapita, na umo katika makucha ya yule mwovu – bali ni nani anayependwa na Mungu, yaani wateule wa Mungu, waliochaguliwa na Mungu, waumini katika Bwana Yesu Kristo wanaounda Kanisa Lake ambalo msingi wake ni wale taifa lililochaguliwa, Israeli halisi, pamoja nao tukiwa sote ni sehemu ya "mbari teule" (Mk. 13;20; 13:22; 13:27; Yoh. 15:16; 15:19; 1Wakor. 1:27-28; 2Tim. 2:10; Tito 1:1; Yak. 2:5).

Ukuhani wa Kifalme (aya ya 9): Katika mjadala wetu wa aya ya 5 hapo juu, tumezungumzia kwa kirefu neema tuliyo nayo sisi waumini kama sehemu ya Bibi Arusi wa Kristo ya kushiriki katika ukuhani wa Bwana wetu; na tunaposhiriki katika vyote alivyo navyo, kwani tu wamoja Naye milele, pia tunashiriki katika Utawala Wake na tutatawala pamoja Naye kwa miaka 1,000 baada ya kurudi Kwake mara ya pili – na milele baada ya hapo. Katika mileniamu, chini ya utawala wa Bwana Yesu Kristo ambaye ameshinda haki ya kuwa na mamlaka haya mawili, yaani kuwa Mfalme wa wafalme na kuwa Kuhani Mkuu, hakutakuwa tena na utengano kati ya mamlaka ya kidunia na mamlaka ya mbinguni kwa sababu ufalme wa Mungu utakuwepo hapa duniani mpaka mwisho wa wakati/majira – nasi tutashiriki katika vipengele vyote hivyo viwili vya Bwana wetu, tukiwa watawala na makuhani, makuhani wafalme, ufalme wa makuhani, "ukuhani wa kifalme" ambao unamwakilisha Mungu kwa wanadamu na kutawala juu ya wanadama kama maofisa wa Mwokozi wetu aliyeshinda (hivyo kutimiza katika taswira zake zote ahadi za kale kwa Israeli ambayo tumekuwa sehemu yake):

6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
Kutoka 19:6 SUV; cf. 61:6

Na ametufanya [sisi] kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba Yake – utukufu na ukuu u na Yeye hata milele na milele. Amina.
Ufu. 1:6 SUV

5.9  Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
5.10  ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao watatawala juu ya nchi.
Ufu. 5:9-10

20.4  Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia [ambao hawakumsujudia] yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
20.6  Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Ufu. 20:4-6
NOTE: Ufunuo 20:5 siyo sehemu ya Neno; iliongezwa na mwandishi asiyejulikana.

Taifa Takatifu (aya ya 9): Wasifu huu wa Kanisa nao pia chimbuko lake ni Israeli kama taifa (Kutoka 19:6). Kwa hakika, taifa la Israeli msingi wake ni imani, Abrahamu akiwa ndiye raia wake wa kwanza na mwanaye Isaka akiendeleza uzao wa imani (Ishmaeli hayumo katika/ndani ya Israeli), na mwana wa kiume wa Isaka aliyeamini, Yakobo, ambaye alipewa jina jipya la "Israeli" na Bwana, akiwa mwenye kupokea neema/baraka (Esau alifungiwa mlango na/kwa uchaguzi wa Mungu kwani aliamua mwenyewe – utashi huru! - kuiuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza wa imani ambao aliudharau). Muda ulivyozidi kwenda katika historia ya taifa hili, ni kweli kwamba wengi katika Israeli wakaonekana kwamba hawana imani ya kiwango cha Abrahamu (War. 9:6), na hivyo hawakuwa sehemu ya "uzao wa ahadi" (War. 4:16). Utakapokuja ufalme pale atakapokuja Bwana wetu, hakutakuwa tena na tofauti kati ya mbari na imani. Kanisa lote, likiwa limefufuliwa na kuchanganywa katika mfumo wa kikabila wa Israeli, litakuwa wakati huo "taifa takatifu" katika kila taswira yake, likiwa limetakaswa kabisa, siyo tu kutokana na nafasi yetu katika Kristo pamoja na [kutakaswa] maishani mwetu tukiwa pamoja na Kristo, bali katika uhitimisho wake, kila memba wa Kanisa akiwa mtimilifu asiye na dhambi milele yote, tukiishi kiuhalisia katika namna ambayo taifa la Israeli la kihistoria halikuweza kufanikisha isipokuwa kwa kufikirika tu (kwa sababu ya hulka ya dhambi ya wanadamu wote) na kinadharia tu (kwa sababu ya uwepo wa utashi huru katika wanadamu wote na matokeo yake yakawa wengi kati ya uzao wa Abrahamu hawakuamua kuwa waumini (War. 7:11; 11:28).

Watu Wanaolindwa (aya ya 9): Pamoja na "ufalme wa makuhani" na "taifa takatifu" , msemo huu pia chimbuko lake ni kitabu cha Kutoka 19:5-6 (mahususi katika aya ya 5), lakini Petro anaiweka neema hii mwishoni. Mzizi wa neno la Kiyunani ambalo linatafsiriwa kama "wanaolindwa/wanaotunzwa" hapa (peripoie – περιποίη-), linahusiana na kutwaa, kutunza na kumiliki, na taswira zote za hizi dhana tatu zimo kwenye matumizi ya Petro ya neno hili hapa. Katika Kiebrania cha Kumbukumbu la Torati 19:5, neno segullah (סְגֻלָּה) maana yake ni "umiliki", kama ilivyo kwa Israeli (na waumini wote katika Kanisa) kuwa ni mali ya Bwana kwa maana maalum. Lakini tunajua kutokana na matumizi ya mzizi wa neno hili katika Agano Jipya kwamba siyo tu umiliki Wake wa sisi waumini Wake unaozungumziwa – na kututwaa Kwake na kutwaa kwetu kwa wokovu kunakotufanya tumilikiwe Naye – bali pia, na mahususi kabisa hapa katika neno hili (peripoiesis/περιποίησίς) maana ya kutunzwa: sisi, Kanisa lililojengwa juu ya Israeli, ni watu tunaotunzwa / tunaolindwa mpaka siku ya mwisho ya wokovu na ufufuo – ambapo hapo tutamtukuza Bwana milele tunapomwabudu Yeye katika milele yote (Luka 17:33; Matendo 20:28; cf. 1Tim. 3:13).

Watakuwa Wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku nitakayowatayarisha wale ninaowamiliki, na nitawaweka mbali na madhara kama vile baba anavyomlinda mwanaye anayemtumikia [kwa uaminifu].
Malaki 3:17

Kuwa sehemu ya "miliki/hazina" ya milele ya Bwana haiwezekani, kwa hakika, bila ya kuwa tumeokolewa na bila ya kuwa tumeshapewa mwili mpya wa milele, "mwili wa ufufuo" ambao kila mmoja wetu akiwa na mwili wake huo mpya, tutaishi na Yeye milele yote. Kwa sababu hii neno hili na kundi [la maneno] yanayotumika nalo katika Agano Jipya karibu kila wakati linarejea ule mwili wa ufufuo na thawabu zinazohusiana nao (ijapokuwa pointi hii muhimu haionekani katika tafsiri na Biblical Commentary mbalimbali, licha ya ukweli kwamba kundi hili la maneno – underlined above – lina neno-mzizi moja mahususi). Kutunzwa na Bwana kwa ajili Yake ili kuwa hazina mahususi Yake na kufaudu mafao yanayotokana na hali hiyo ni suala la urithi wetu wa milele:

(13) Katika [Kristo] ninyi pia mlipolisikia Neno la ile kweli, habari njema za wokovu wenu, na mkaamini katika Yeye, mkatiwa muhuri na Roho wa ahadi, Roho [Mtakatifu],
(14) ambaye ndiye dhamana ya urithi wetu (urithi ulio na msingi wake katika mwili wa ufufuo) kwa ajili ya kuugomboa/kudhamini utunzwaji wa [urithi huo] (yaani, peripoiesis / περιποίησις – kutunza/kulinda ufufuo na thawabu yetu), kwa sifa ya utukufu Wake.
Waefe. 1:13-14

AU (Tafsiri nyingine):

(13) Katika Yeye nanyi pia, mlipolisikia neno la [ile] kweli, Injili ya wokovu wenu, na mkaamini katika Kristo, mkatiwa muhuri wa ahadi wa Roho Mtakatifu,
(14) ambaye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoutwaa [urithi huo], kwa sifa ya utukufu Wake.
Waefe. 1:13-14 (kutoka ESV Bible)

(9) Kwa kuwa Mungu hakututeua tupitie ghadhabu Yake, bali kwa ajili ya kutwaa ( peripoiesis / περιποίησις) wokovu wetu (katika ufufuo) kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
(10) Yeye aliyekufa kwa ajili yetu, ili kwamba, tukiwa hai au tukiwa katika usingizi (kifo cha mwili huu wa sasa), tutakuwa wazima pamoja na Yeye (katika siku ya ufufuo).
1Wathess. 5:9-10

(14) Kwani ni kwa kusudi hili (wokovu kwa njia ya utakaso wa Roho na imani katika kweli; aya ya 13) Yeye aliwaita kwa njia ya Injili yetu ili mpate kutwaa (peripoiesis / περιποίησις) utukufu wa milele (ufufuo) wa (utokao kwa) Bwana wetu Yesu Kristo.
2Wathess. 2:14

(39) Lakini sisi hatuna woga unaosababisha uasi [ambao nao] unapelekea kwenye uharibifu, bali tunayo imani inayopelekea kwenye kutunzwa ( peripoiesis / περιποίησις) kwa uzima wetu wa milele (katika ufufuo).
Waebr. 10:39

Mpate Kuzitangaza Fadhili (Uadilifu) Zake (aya ya 9): Kama vile jina "uzao / mbari teule" lilivyotoka katika Kitabu cha Isaya, msemo huu pia unatoka katika sura hiyo hiyo, mahususi katika 43:21. Hata hivyo, Petro anapewa uwezo na Roho Mtakatifu wa kuunganisha moja kwa moja matendo yetu ya kutangaza utukufu wa Mungu na mfululizo wa mafao (baraka) ambayo tumeyapokea kutoka Kwake, kwa kutumia msemo wa "lengo/kusudi lake ni ...". Kwa maneno mengine, lengo la Mungu katika kutufanya sisi, "uzao/mbari teule", "makuhani wa kifalme", "taifa teule", na "watu wanaolindwa/wanaotunzwa" ni mahususi: kushuhudia wema, uadilifu na utukufu wa Mungu.

6 Mimi, Bwana, nimekuita katika haki [uongofu], nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa [kukuteua] uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;
Isaya 42:6

Aya hii, ambayo inatoa unabii kuhusu ujio wa kwanza wa Bwana wetu na kupanuka na kuenea kwa kiasi kubwa kwa wokovu hata [kufika] katika mataifa yote ya duniani (Isa. 49:6; Matendo 13:47; 26:23), pia inatumika kwa taifa la Israeli lenyewe. Kama ambavyo ulimwengu ulitakiwa kumwona Bwana katika ushuhuda wa watu Wake Israeli, vivyo hivyo ulimwengu unapaswa kumwona Bwana akiakisiwa katika maneno na matendo ya watu wote walio ndani ya Kanisa Lake. Hata hivyo, kama vile Israeli ilivyoshindwa kufikia upeo huu kama taifa, vivyo hivyo sisi Wakristo tunapaswa kuwa waangalifu tusije tukashindwa kufikia upeo wetu kila mmoja wetu peke yake. Kukua kiroho ni lazima ili kutimiza agizo hili. Kutangaza "uadilifu" au "ubora kabisa" (katika Kiyunani ni arete) wa Mungu – shani ya hulka Yake timilifu na matendo Yake yaliyojaa neema kwetu na kwa ulimwengu (kwanza kabisa katika dhabihu ya Bwana Yesu Kristo msalabani) – kunastahili zaidi ya kumpa Yeye maneno matupu tu, na kuyapa matendo Yake maneno matupu pia. Kwani kitu muhimu siyo kwamba tunasema, bali tunasema nini na tunakisema namna gani – na pia ni "nani" hao wanaosema ni suala muhimu pia. Mkristo ambaye yuko hatua moja tu kuelekea kwenye matokeo ya kutisha ya dhambi ya mauti (1Yoh. 5:16) ambaye anajihusisha na kila aina ya matendo maovu hawezi kuwa na ushuhuda sahihi/stahiki wa utukufu wa Mungu – hata kama anazisema sifa hizo katika namna sahihi. Zaidi ya hapo, si maneno yetu tu yaliyo na umuhimu, bali pia matendo yetu yana umuhimu mkubwa. Kama Yakobo anavyotilia mkazo, haina faida yoyote kusema maneno ya sifa ambayo mara yanaonyeshwa kuwa ni matupu kutokana na matendo mabaya ya msemaji yasiyoendana na maneno hayo (Yakobo 2:14-17). Hivyo kutotoa maneno ya sifa kwa Bwana ni tatizo kama ilivyo kutoa maneno ya sifa katika namna isiyostahili ni tatizo pia – na kushindwa kuwapa wale wanaotutazama kwa makini, wanadamu na malaika, ushuhuda wa maisha ambao unadhihirisha wema, huruma, upendo na utukufu wa Mungu yaweza kuwa ni tatizo kubwa zaidi ya yote, kwani ni dalili ya kutokuwepo kwa upevu wa kiroho, maendeleo ya kiroho na utumishi/kuzaa matunda, vitu ambavyo ndivyo vinajumuisha lengo la maisha yetu hapa duniani baada ya wokovu.

3.17  Basi <Bwana> ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
3.18 Na kila mmoja wetu, ikiwa tutaakisi utukufu wa Bwana bila “utaji” unaofunika nyuso zetu (yaani kwa ushuhuda safi wa Kikristo), tunabadilishwa na tunakuwa na taswira hiyo hiyo (tunazidi kuwa kama Kristo) na hivyo kuakisi utukufu unaoongezeka zaidi na zaidi – kama inavyotarajiwa ikiwa Roho wa Bwana ndiye wakala wa mabadiliko yetu.
2Wakor. 3:17-18

Kwa kuwa tunaye Roho wa Bwana anayetusaidia katika haya yote, na kwa kuwa tumepewa karama ya wingi wa neema kwa lengo hilo, yaani kuchaguliwa na Mungu kwa ajili ya uzima wa milele, kufanywa makuhani wa kifalme wa Mungu Mkuu, kusogezwa karibu ili tuwe sehemu ya taifa takatifu na kujumuishwa na watu Wake ili tutunzwe na kulindwa mpaka tutakapofufuliwa na kuthawabiwa – basi na tusilegeze kamba katika kudhihirisha ubora wa hali ya juu wa Mungu katika kila kitu tunachokifikiri na tunachokisema na tunachokifanya, na badala yake tuitikie wito unaodhihirishwa na neema zisizo kifani tulizopewa katika namna ambayo Bwana wetu mpendwa anataka. Kama ambavyo Yeye ndiye "nuru ya ulimwengu" (Yoh. 8:12; 9:5), vivyo hivyo sisi tunapaswa "kuakisi" nuru hii ambayo ndiyo ujumbe, Neno la wokovu, tunapotoa sifa Kwake na kuitikia kwa shukrani wito Wake na kwa neema Yake kwetu katika kila tunalokiri, tunalosema na tunalofanya – ili kumletea Yeye na Baba yetu aliye mbinguni sifa zote stahili.

5.14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika [yaani, kufichika – hidden] ukiwa juu ya mlima.
5.15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango (i.e. lampstand); nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
5.16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Matt. 5:14-16

Kwani kwa hali yoyote ile, tutakuwa tukitekeleza agizo hili la kutoa sifa milele yote.

4 Heri wenye kudura/majaliwa ya kukaa nyumbani mwako, [kwani hao] Watakuhimidi daima.
Zab. 84:4

... zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake adhimu (aya ya 9): Huu ni ulimwengu wa giza, uliojaa hofu na ukosefu wa tumaini. Lakini Mungu ameifanya nuru Yake kung'ara na kuiangaza katika nafsi ya Bwana Yesu Kristo, Yeye aliye "Nuru ya ulimwengu" (Isa. 42:6; 49:6; Yoh. 8:12; 9:5; 12:46; cf. Isa. 9:2; 10:17; Yoh. 1:4-5; 1:9).

1.12  mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu [yenu] ya urithi wa watakatifu katika nuru [ya milele].
1.13  Naye alituokoa [kutoka] katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa;
Wakol. 1:12-13

Kuwa na uzima wa milele badala ya mauti, tumaini la ufufuo badala ya hofu ya hukumu, na nuru ya kweli badala ya uwongo wa giza la ulimwengu huu, ni jambo stahiki, basi tumpe sifa Yeye aliyetuita kutoka gizani na kutuleta katika nuru ya utukufu wa Yesu Kristo, Bwana wetu na Mwokozi wetu. Mungu Baba alituita, na hivyo imeandikwa katika Mpango Wake kwamba amefanya hivyo (War. 8:28-30), kwa msingi wa itikio chanya Aliloliona tangu milele iliyopita. Kuitwa kwetu katika nuru ya kweli na katika uzima wa milele ambao kwa sasa tunao kwa sababu tu ya nafasi tuliyo nayo katika Bwana Yesu Kristo pia kunatazamia kutukuzwa kwetu pale tutakapokuwa "nuru katika Bwana" kwa kila namna (Waefe. 5:8; cf. Zab. 73:24). Katika ile siku tukufu ijayo sote tutaijua kweli "kama vile nasi tutakavyojulikana" Naye (1Wakor. 13:12). Hadi siku hiyo basi, ebu tuendelee kuikumbatia nuru ya kweli ambayo kwayo tumeokolewa ili tuendelee na mwendo wetu na Bwana katika nuru, tukikanusha kila uwongo na tukiakisi nuru ya utukufu wake Yeye aliyetugomboa kwa uhai Wake.

5.8  Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
5.9  Sasa, tunda linalotokana na nuru huendana na wema, haki/uongofu na kweli yote
5.10  katika kila kitu mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
5.11  Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali [myafichue na] myakemee;
5.12  kwa kuwa yanayotendeka kwa siri na wale walioikataa kweli, ni aibu hata kuyanena.
5.13  Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.
5.14  Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.
Waefe. 5:8-14

Sasa Mmekuwa Taifa (aya ya 10): Kama vile Petro alivyowaambia wasomaji wake mwanzoni kabisa mwa waraka wake, ijapokuwa walikuwa "wametengwa na jamii", sasa wao na sisi pia "tumeteuliwa" ili tuwe watu wa Bwana Yesu Kristo kwa njia ya dhabihu Yake kwa ajili yetu. Aya hii imeundwa katika mfumo wa mizani ya shairi lenye beti mbili (kulingana na jadi za mashairi za Kiebrania zaidi kuliko zile za Kiyunani na Kirumi), hivyo kwamba huu siyo tu msisitizo wa pili wa dhana ambayo Petro alikwishaifundisha katika aya iliyopita, bali ni siafa ya kazi tukufu ya Mungu aliyoifanya katika kuwaita watu kwa ajili Yake kutoka kwa Wayahudi na watu wa mataifa pia. Ni neema kubwa kumwona Petro hapa, yule mtume wa "wenye tohara" (Wagal. 2:7-8), na ambaye alihitaji maelekezo ya kina haswa, pamoja na "kusukumwa" na kutiwa moyo na Roho Mtakatifu ili hata akubali kuonana tu na watu wa mataifa (Matendo. 10:10-16), na ambaye hata hivyo hakuwa "mkamilifu" kivile katika kujituma katika suala hili (Wagal. 2:11-14), sasa akifurahi kwa moyo wake wote katika wokovu wa watu wa mataifa ambao sasa amekuwa mtume wao katika kila maana ya neno "mtume". Kufikia wakati huu, Paulo alikuwa amekwishauawa kwa imani yake, lakini Petro alibeba majukumu yake [Paulo] katika Asia Ndogo ili aweze kuvuna mavuno mengi kati ya watu wa mataifa pia:

2.11 Hivyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa mataifa, mkiitwa "wale wasiotahiriwa" na wale walio uzao wa tohara ya kimwili na iliyofanywa na wanadamu.
2.12 Kumbukeni kwamba mlikuwa bila Kristo, mliotengwa na dola ya Israeli, msioshirikishwa katika maagano [yake] ya ahadi, bila matumaini na bila Mungu hapa duniani.

2.13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi ambao mlikuwa mbali kabisa mmeletwa karibu kwa damu ya Kristo.
Waefe. 2:11-13

Sasa Mmepata Rehema (aya ya 10): Kama ilivyo katika ushairi wa Kiebrania (soma tu kitabu cha Mithali, uone), ubeti wa pili unaufafanua, na unaenda sambamba na, ubeti wa kwanza. Katika beti zote mbii, sehemu ya pili ya kila ubeti inadhihirisha kwa kutofautisha na ule [ubeti] wa kwanza yale mabadiliko [ma]tukufu yaliyowatokea wasomaji/walengwa wa waraka wa Petro (na sisi pia). Wakati fulani "hawakuwa [hata] taifa", lakini sasa wamekuwa "watu wa Mungu". Vivyo hivyo hapa, wao na sisi na waumini wote hapo zamani tulikuwa wote walengwa wa ghadhabu ya Mungu (Waefe. 2:3; cf. War. 1:18), lakini sasa tumesamehewa na tumepokea na tunafurahia utukufu katika huruma ya Mungu tuliyoipokea katika wokovu (Waefe. 2:4-7; 1Wathess. 5:19). Huruma, tunapaswa kuona, ni tafsiri ya neno la Kiyunani eleos (ambalo nalo linatangamana na neno la Kiyunani chezedh), na ni "baraka-daraja" linaloziunganisha neema za Mungu na/kwa amani/ukamilifu/baraka tulizo nazo katika Mungu kama matokeo ya wokovu (1Tim. 1:2; Tito 1:4; 2Yoh. 1:3): katika neema Zake, Mungu anatoa jibu/ufumbuzi kwa tatizo la dhambi ambalo vinginevyo litatutia katika hukumu/hatia – na Anafanya hivyo kwa gharama kubwa kuliko zote Kwake Mwenyewe; matokeo ya wokovu ni sisi kuwa na amani ya Mungu – kuondolewa kwa ghadhabu na hukumu/hatia na kurejeshwa katika uhusiano wa neema ambao ni wa shani kubwa sasa hivi, na usio na kifani pindi tutakapomaliza dahari hii na kuingia katika milele; katika wokovu (maisha yetu hapa duniani, kabla ya ufufuo), neema ya Mungu inakutana na mapokezi yetu (kama viumbe wenye dhambi, wasiostahili) ya toleo Lake la wokovu huo kwa imani, na hapo tunaiona huruma ya Mungu. Hatukuwa na kitu chochote tunachoweza kukileta mbele Yake ili kurejesha amani na usuluhisho kati yetu na Yeye, hivyo Yeye amefanya/ametoa kila kitu: dhabihu ya Bwana Yesu Kristo msalabani katika kifo chake cha kiroho ili kulipia dhambi zetu zote. Tunachokifanya sisi ni kupokea zawadi hii yenye neema kuu kwa kumtegemea Yeye , Mwokozi wetu, na kile alichokifanya kwa ajili yetu katika kulipia gharama ya kutugomboa ambayo sisi wenyewe hatukuweza na hatuwezi kuilipa.5 Hivyo ndivyo tunavyoipokea huruma ya Mungu ambayo inatokana na neema Yake na, matokeo yake, tunafaudu amani ya uhusiano uliorejeshwa kati yetu na Yeye katika Bwana Yesu Kristo kama watoto wa Mungu aliye juu.6 Hakuna kitu hapa duniani chenye shani zaidi ya kuokolewa kutoka dhambi na kifo ... na kufanywa sehemu ya familia ya Mungu Mwenyewe badala yake. Si jambo la kushangaza basi, kuona kwamba Petro aliona ni sahihi kuweka kumbukumbu ya ukweli huu katika namna hii ya pekee:

2.10 ninyi ambao hapo mwanzo hamkuwa taifa,
lakini sasa mmekuwa taifa la Mungu;
ninyi ambao hapo mwanzo hamkupata rehema,
lakini sasa mmepata rehema.
1Petro 2:10

Toleo hili la rehema (ya bure) katika kuokolewa kutoka dhambi na upatanisho na Mungu unaweza kupatikana kwa wanadamu wote kwa njia ya kifo cha kiroho cha Bwana Yesu Kristo kwa niaba yetu sote. Sifa ziende kwa Mungu kwa sababu sisi tunaoamini tumepata neema ya kupokea zawadi hii kuu kwa njia ya imani [rahisi] katika Kristo, Yeye aliyeacha kila kitu [kule mbinguni] ili aje hapa duniani na kutuokoa na kifo! Hivyo basi tufanye juhudi zote kuitumia hii neema kuu kuliko zote - pamoja na neema nyingine kubwa na za ajabu zinazotokana nayo na zilizoelezwa hapo juu katika aya mbalimbali – kwa kuendelea kukua kiroho, kuendelea na mchakato wa kupevuka, na kuendelea na mchakato wa kuzaa matunda, kwa ajili ya utukufu wa Yule Mmoja ambaye tunampenda zaidi ya maisha yetu, mpendwa wetu, Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Notes:

1. Hii ni kweli pia popote pale orodha ya maadili (matendo mema) inapofundishwa, kama kwa mfano katika Zab. 15:1-5 au 2Pet. 1:5-9.

2. Petro anafuata tafsiri ya Septuagint (LXX) lakini si neno-kwa-neno, bila shaka kwa ajili ya/sababu wasomaji wake walikwishaizoea tafsiri hii ya Kiyunani ya Agano la Kale. Kitenzi cha Kiebrania chush, ambacho kwa ujumla hutumika kuhusiana na watu na kinamaanisha "kufanya haraka", kinatumika kitamathali (figuratively au kimethali) hivyo kwamba "kutingishwa" ni tafsiri inayoweza kutetewa (kuwa defended). "Hatatetemeka na/kwa hofu" yaweza kuwa namna mojawapo, katika kiswahili, ya kuelezea tatizo la kimwili na la ki-hisia, ambalo linadokezwa na kitenzi-neno hiki.

3. Ili kupata orodha ya faida kubwa zinazoongezeka kwa waumini wote walioa katika umoja wa Kristo, tizama sehemu ya III ya Bible Basics 4B: Soteriology: "What it Means to be Saved".

4. Tumeona pia katika sehemu nyingine kwamba baada ya historia kupita (yaani tukiingia katika milele), waumini wa Enzi ya Kanisa ambao sio wa uzao (damu) wa Israeli watachanganywa kila mmoja wao katika moja ya makabila yake, kutegemea na jinsi tulivyoitikia wito wa Bwana wetu katika maisha yetu hapa duniani. Tazama sehemu ya 5 ya The Satanic Rebellion, Section II.8.C, The Jewish Ceremonial Calendar", under Israel: The Ultimate Organization".

5. Tizama sehemu ya II ya Bible Basics 4A: Christology "The Saving Work of Jesus Christ" Section 7, Redemption".

6. Tizama sehemu ya II ya Bible Basics 4A: Christology: "The Saving Work of Jesus Christ", sehemu ya 9, "Reconciliation".

=0=

Imetafsiriwa kutoka: Three Analogies for the Christian Life: Peter's Epistles #33

=0=

Basi, na tuonane katika somo #34 la mfululizo huu, kwa neema ya Mungu, Amen!